Psalms 35:1-6

Kuomba Msaada: Kuokolewa Kutokana Na Maadui

(Zaburi Ya Daudi)


1 aEe Bwana, pingana na wale wanaopingana nami,
upigane na hao wanaopigana nami.

2 bChukua ngao na kigao.
Inuka unisaidie.

3 Inua mkuki wako na fumo
Fumo ni sawa na sagai, maana yake ni mkuki mfupi.
lako
dhidi ya hao wanaonifuatia.
Iambie nafsi yangu,
“Mimi ni wokovu wako.”


4 dWafedheheshwe na waaibishwe
wale wanaotafuta uhai wangu.
Wanaofanya shauri kuniangamiza
warudishwe nyuma kwa hofu.

5 eWawe kama makapi yapeperushwayo na upepo,
malaika wa Bwana akiwafukuza.

6 Njia yao na iwe giza na ya utelezi,
malaika wa Bwana akiwafuatilia.
Copyright information for SwhKC